SAKRAMENTI YA EKARISTI
Na. 1323 - mwokozi wetu katika karamu ya mwisho usiku alipotolewa aliweka sadaka ya ekaristi ya mwili na damu yake. Alifanya hivyo ili kuendeleza sadaka ya msalaba siku zote mpaka atakaporudi, kusudi amwachie bibi arusi mpendwa yaani kanisa ukumbusho wa kifo chake na ufufuko wake sakramenti ya upendo, umoja, kifungo cha mapendo, karamu ya pasaka ambamo Kristo huliwa na roho hujazwa neema na ambamo tunapewa amana ya uzima wa milele.
Na. 1324 - Ekaristi ni chemichemi na kilele cha maisha yote ya kikristo. Sakramenti nyingine kama zilizo pia huduma zote za kanisa na kazi za utume zaungana na ekaristi na zaelekezwa kwake. Kwani katika ekaristi takatifu mna kila hazina ya kiroho ya kanisa yaani kristo mwenyewe pasaka wetu.
Na. 1325 - Ekaristi ndio ishara thabiti na sababu ya hali ya juu kabisa ya ushirika katika uzima wa kimungu na umoja ule wa taifa la Mungu ambao unalifanya kanisa liwepo ekaristi ni kilele cha tendo la Mungu la kuutakatifuza ulimwengu katika kristo na kilele cha tendo la kumwabudu Mungu wampalo watu kristo na kwa njia yake wampalo baba katika mtakatifu.
Na. - 1326 - mwishowe kwa njia ya adhmisho la ekaristi tunaungana tayari sisi wenyewe na liturjia ya mbinguni na tunaanza kutangualia kushiriki uzima wa milele Mungu atakapokuwa yote katika wote - 1 Kor. 15:28 - basi vitu vyote vikiisha kutiishwa chini yake ndipo mwana mwenyewe naye atatiishwa chini yake yeye aliyemtiisha vitu vyote ili kwamba Mungu awe yote katika wote.
Na. - 1327 - kwa ufupi ekaristi ndiyo juma na muhtasari wa imani yetu, namna yetu ya kufikiri hulingana na ekaristi na ekaristi kwa zamu yake huimarisha namna yetu ya kufikiri.
BAADHI YA PICHA SIKU YA MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA EKARISTI TAKATIFU KATIKA PAROKIA YA MT. MAXMILIAN MARIA KOLBE MWENGE 2016.
Mama Paschal, mwimbaji kwaya ya Mt. Augustino Mwenge.
Glory Mlembe, mwimbaji kwaya ya Mt. Augustino Mwenge.
Mr. Makene, mwimbaji kwaya ya Mt. Augustino Mwenge.
Mr. George, mwimbaji kwaya ya Mt. Augustino Mwenge.
Mr. Deligo, mwimbaji kwaya ya Mt. Augustino Mwenge.
Mr. Adam, mwimbaji kwaya ya Mt. Augustino Mwenge.
Wapiga Ngoma wakipiga ngoma kwa madaha kabisa.
Watoto wakimwaga maua wakisafisha njia.
Baadhi ya wanakwaya wa mt. Boromeo.
Ndugu Chrispin akifanya yake.
Utoto mtakatifu mwenge.
Mwenyekiti wa Parokia ya mwenge Paroko Fr. Eugene SDs.
Baadhi ya wanakwaya wa mt. Cecilia Mwenge.
Masista.
Baadhi ya wanakwaya ya Mt. Augustino Mwenge.
0 comments:
Post a Comment